Msaada wa Masomo
Yesu Kristo


Yesu Kristo

Kristo (neno la Kiyunani) na Masiya (neno la Kiebrania) maana yake ni “mpakwa mafuta.” Yesu Kristo ndiye Mzaliwa wa kwanza wa Baba katika roho (Ebr. 1:6; M&M 93:21). Yeye ndiye Mzaliwa Pekee wa Baba katika mwili (Yn. 1:14; 3:16). Yeye ndiye Yehova (M&M 110:3–4) na aliteuliwa katika wito wake mkuu kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Chini ya maelekezo ya Baba, Yesu aliumba dunia na kila kitu kilichopo juu yake (Yn. 1:3, 14; Musa 1:31–33). Alizaliwa na Maria huko Bethlehemu, aliishi maisha yasiyo na dhambi, na akafanya upatanisho kamili kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote kwa kumwaga damu Yake na kwa kutoa uhai Wake juu ya msalaba (Mt. 2:1; 1 Ne. 11:13–33; 3 Ne. 27:13–16; M&M 76:40–42). Akafufuka kutoka kwa wafu, hivyo akathibitisha hatima ya kufufuka kwa wanadamu wote. Kupitia Upatanisho na Ufufuko wa Yesu, wale wanaotubu dhambi zao na kutii amri za Mungu wanaweza kuishi milele pamoja na Yesu na Baba (2 Ne. 9:10–12; 21–22; M&M 76:50–53, 62).

Yesu Kristo ndiye mtu mkuu kuliko wote waliozaliwa juu ya dunia. Maisha Yake ni mfano kamili wa jinsi wanadamu wote itupasavyo kuishi. Sala, baraka, na ibada zote za ukuhani zinapaswa kufanyika katika jina Lake. Yeye ni Bwana wa mabwana, Mfalme wa wafalme, Muumba, Mwokozi, na Mungu wa dunia nzima.

Yesu Kristo atakuja tena katika uwezo na utukufu ili kutawala juu ya dunia wakati wa Milenia. Katika siku ya mwisho, yeye atawahukumu wanadamu wote (Alma 11:40–41; JS—M 1).

Muhtasari wa maisha Yake (katika mfuatano wa matukio)

Kichwa cha Kanisa

Kujichukulia jina la Yesu Kristo juu yetu

Kuonekana kwa Kristo baada ya kifo

Kuwepo kwa Kristo kabla ya kuzaliwa duniani

Mamlaka

Mfano wa Yesu Kristo

Mifano au ishara za Kristo

Mwamuzi

Unabii juu ya Kuzaliwa na Kifo cha Yesu Kristo

Ushuhuda uliotolewa juu ya Yesu Kristo

Utawala wa Kristo katika milenia

Utukufu wa Yesu Kristo