Misaada ya Kujifunza
Galilaya


Galilaya

Katika nyakati za zamani na za kisasa hii ni wilaya ya kaskazini kabisa ya Israeli magharibi ya Mto Yordani na bahari ya Galilaya. Galilaya ina ukubwa upatao maili sitini (kilometa tisini na saba) urefu wa maili thelathini (kilometa arobaini na nane) upana. Hapo zamani ilikuwa na ardhi iliyokuwa bora na miji iliyokuwa na shughuli nyingi zaidi katika Israeli. Barabara kubwa muhimu zinazoelekea Dameski, Misri, na Israeli ya mashariki zilipitia Galilaya. Hali yake ya hewa nzuri na udongo wenye rutuba ilizaa mazao mengi ya mizeituni, ngano, shayiri, na zabibu. Uvuvi katika bahari ya Galilaya ulitoa biashara kubwa ya kusafirisha nje ya nchi na ilikuwa ni chanzo kikubwa cha utajiri. Mwokozi alitumia muda wake mwingi katika Galilaya.

Bahari ya Galilaya

Bahari ya Galilaya iko katika Israeli ya kaskazini. Pia katika Agano la Kale ilikuwa ikiitwa Bahari ya Kinerethi na Ziwa la Genesareti au Tiberia katika Agano Jipya. Yesu alifundisha mahubiri kadhaa mahali hapo (Mt. 13:2). Bahari hii ina umbile la pea, maili 12.5 (kilometa 20) urefu na maili 7.5 (kilometa 12) upana, katika mapana yake makubwa. Iko futi 680 (mita 207) chini ya usawa wa bahari, ambayo mara kwa mara hufanya hewa inayolizunguka kuwa na joto kali. Hewa baridi inayoteremka kutoka vilimani na kukutana na hewa ya joto juu ya maji mara kwa mara husababisha tufani (Lk. 8:22–24).