Misaada ya Kujifunza
Efraimu


Efraimu

Katika Agano la Kale, huyu ni mwana wa pili wa Yusufu na Asinathi (Mwa. 41:50–52; 46:20). Kinyume na taratibu za kimila, Efraimu alipokea baraka ya haki ya uzaliwa wa kwanza badala ya Manase, ambaye ndiye alikuwa mwana mkubwa (Mwa. 48:17–20). Efraimu akawa baba wa kabila la Efraimu.

Kabila la Efraimu

Efraimu alipewa haki ya uzaliwa wa kwanza katika Israeli (1 Nya. 5:1–2; Yer. 31:9). Katika siku za mwisho nafasi yao na wajibu wao ni kuushikilia ukuhani, kupeleka ujumbe wa injili ya urejesho kwa ulimwengu, na kuipeperusha bendera ili kuwakusanya Israeli waliotawanyika (Isa. 11:12–13; 2 Ne. 21:12–13). Watoto wa Efraimu watawavisha taji pamoja na utukufu wale watokao nchi za kaskazini wanaorejea katika siku za mwisho (M&M 133:26–34).

Kijiti cha Efraimu au Yusufu

Historia ya kikundi kimoja kutoka kabila la Efraimu ambacho kiliongozwa kutoka Yerusalemu hadi Marekani karibu miaka 600 K.K. Historia ya kikundi hiki inaitwa kijiti cha Efraimu au Yusufu au Kitabu cha Mormoni. Hiki na kijiti cha Yuda (Biblia) huunda ushuhuda wa pamoja wa Bwana Yesu Kristo, Ufufuko Wake, na kazi Yake takatifu miongoni mwa sehemu hizi mbili za nyumba ya Israeli.