Misaada ya Kujifunza
Nyoka wa shaba nyeupe


Nyoka wa shaba nyeupe

Nyoka wa shaba nyeupe aliyetengenezwa na Musa kwa amri ya Mungu ili kuwaponya Waisraeli ambao walikuwa wameumwa na nyoka wakali (nyoka wenye sumu) nyikani (Hes. 21:8–9). Nyoka huyu wa shaba nyeupe alitundikwa kwenye mlingoti na “kuinuliwa juu ili kwamba mtu yeyote ambaye angeliangalia apate kuishi” (Alma 33:19–22). Bwana alielezea kwa kuinuliwa kwa yule nyoka nyikani kama ni ishara yake Yeye mwenyewe akiwa ameinuliwa juu ya msalaba (Yn. 3:14–15). Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha historia juu ya nyoka wakali na jinsi watu walivyokuwa wameponywa (1 Ne. 17:41; 2 Ne. 25:20; Hel. 8:14–15).