Misaada ya Kujifunza
Nefi, Mwana wa Nefi, Mwana wa Helamani


Nefi, Mwana wa Nefi, Mwana wa Helamani

Mmoja wa wale wanafunzi Wanefi kumi na wawili waliochaguliwa na Yesu Kristo mfufuka katika Kitabu cha Mormoni (3 Ne. 1:2–3; 19:4). Nabii huyu alisali kwa bidii sana kwa Bwana kwa niaba ya watu wake. Nefi aliisikia sauti ya Bwana (3 Ne. 1:11–14). Nefi pia alitembelewa na malaika, aliwafukuza pepo wabaya, alimfufua kaka yake kutoka kwa wafu, na alitoa ushuhuda ambao hangeweza kukosa kuaminika (3 Ne. 7:15–19; 19:4). Nefi alitunza kumbukumbu ya kimaandiko (3 Ne. 1:2–3).

Kitabu cha 3 Nefi

Kitabu kilichoandikwa na Nefi, mwana wa Nefi, katika Kitabu cha Mormoni. Mlango wa 1–10 inaonyesha kutimilika kwa unabii juu ya kuja kwa Bwana. Ishara ya kuzaliwa kwa Kristo ilitolewa; watu wakatubu; lakini wakarudi kwenye uovu. Mwishowe tufani, matetemeko ya ardhi, dhoruba kali, na maangamizo makubwa yalikuwa ishara ya kifo cha Kristo. Mlango wa 11–28 inaandikwa ujio wa Kristo katika Marekani. Hii ndiyo sehemu muhimu ya Kitabu cha 3 Nefi. Maneno mengi ya Kristo yanafanana na mahubiri Yake yaliyoandikwa katika Biblia (kwa mfano, Mt. 5–7 na 3 Ne. 12–14). Mlango wa 29–30 ni maneno ya Mormoni kwa mataifa ya siku za mwisho.

Kitabu cha 4 Nefi

Kitabu hiki kina aya arobaini na tisa tu, zote ni katika mlango mmoja, hata hivyo inaelezea taarifa za karibu miaka mia tatu ya historia ya Wanefi (34–321 B.K.). Waandishi wa vizazi kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na Nefi, walichangia katika kumbu kumbu hii. Mstari wa 1–19 inazungumzia kwamba baada ya kuja kwa Kristo mfufuka Wanefi na Walamani wote waliongolewa katika injili. Amani, upendo, na maelewano vilitawala. Wanafunzi Wanefi watatu, ambao Kristo aliwaruhusu kubakia duniani hadi Ujio Wake wa Pili (3 Ne. 28:4–9), waliwahudumia watu. Nefi aliacha kumbukumbu hiyo kwa mwanawe Amosi. Mstari wa 19–47 ni kumbukumbu za utumishi wa Amosi (miaka 84) na ule wa mwanawe Amosi (miaka 112). Katika mwaka 201 B.K. kiburi kikaanza kusababisha matatizo miongoni mwa watu, ambao waligawanyika wenyewe katika madaraja na wakaanzisha makanisa ya uongo ili kupata faida (4 Ne. 1:24–34).

Mstari ya mwisho ya 4 Nefi inaonyesha kwamba watu walikuwa wamerudia tena kwenye uovu (4 Ne. 1:35–49). Katika mwaka 305 B.K., Amosi mwana wa Amosi alikufa na kaka yake Amaroni akazificha kumbukumbu takatifu zote kwa usalama. Amaroni baadaye alizikabidhisha kumbukumbu hizo kwa Mormoni, ambaye aliandika matukio mengi ya wakati wa uhai wake na kisha akazifanyia muhtasari (Morm. 1:2–4).