Misaada ya Kujifunza
Nuru, Nuru ya Kristo


Nuru, Nuru ya Kristo

Nguvu za kiungu, uwezo, au ushawishi unaotokana na Mungu kupitia kwa Kristo na kutoa uhai na nuru kwa vitu vyote. Ni sheria ambayo kwayo vitu vyote vinatawaliwa mbinguni na duniani (M&M 88:6–13). Pia huwasaidia watu kuelewa kweli za injili na husaidia kuwaweka katika njia ile ya injili ambayo huwaongoza kwenye wokovu (Yn. 3:19–21; 12:46; Alma 26:15; 32:35; M&M 93:28–29, 31–32, 40, 42).

Nuru ya Kristo isifananishwe pamoja na Roho Mtakatifu. Nuru ya Kristo siyo mtu. Ni ushawishi utokao kwa Mungu na kumtayarisha mtu kumpokea Roho Mtakatifu. Ni ushawishi wa kutenda mema katika maisha ya watu wote (Yn. 1:9; M&M 84:46–47).

Onyesho moja la nuru ya Kristo ni dhamiri, ambayo humsaidia mtu kuchagua kati ya mema na mabaya (Moro. 7:16). Kadiri watu wanavyojifunza zaidi juu ya injili, dhamiri zao huwa nyepesi zaidi katika kuhisi (Moro. 7:12–19). Watu wanaoifuata nuru ya Kristo huongozwa kwenye injili ya Yesu Kristo (M&M 84:46–48).