Msaada wa Masomo
Dhamiri
iliyopita inayofuata

Dhamiri

Hisia ya ndani kabisa ya sahihi na baya, inayokuja kutokana na Nuru ya Kristo katika wanadamu wote (Moro. 7:16). Tunazaliwa tukiwa na uwezo wa asili wa kutofautisha kati ya mema na mabaya kwa sababu ya Nuru ya Kristo ambayo hutolewa kwa kila mtu (M&M 84:46). Uwezo huu unaitwa dhamiri. Kuwa nayo ndiyo hutufanya sisi kuwa viumbe wenye kuwajibika. Kama uwezo mwingine, dhamiri zetu zaweza kudhoofishwa kwa njia ya dhambi au matumizi mabaya.