Misaada ya Kujifunza
Agano Jipya na Lisilo na Mwisho


Agano Jipya na Lisilo na Mwisho

Utimilifu wa injili ya Yesu Kristo (M&M 66:2). Ni mpya kila wakati inapofunuliwa upya kufuatia kipindi cha ukengeufu. Ni lisilo na mwisho katika maana ya kwamba ni Agano la Mungu na limekuwa likifurahiwa katika kila kipindi cha maongozi ya injili ambapo watu wamekuwa radhi kuipokea. Agano jipya na lisilo na mwisho lilifunuliwa tena kwa wanadamu duniani na Yesu Kristo kupitia Joseph Smith Nabii. Inazo ibada takatifu zinazoendeshwa kwa mamlaka ya ukuhani—kama vile ubatizo na ndoa ya hekaluni—ambazo humpa mwanadamu wokovu, mwili usiokufa, na uzima wa milele. Watu wanapoikubali injili na kuahidi kushika amri za Mungu, Mungu hutoa agano na kuwapa baraka za agano Lake jipya na lisilo na mwisho.