Misaada ya Kujifunza
Agano la Kale


Agano la Kale

Maandishi ya manabii wa kale waliofanya hivyo chini ya ushawishi wa Roho Mtakatifu na ambao kwa karne nyingi walimshuhudia Kristo na huduma Yake ya wakati ujao. Pia linayo kumbu kumbu ya historia ya Ibrahimu na uzao wake, ikianzia na Ibrahimu, na agano, au ushuhuda, ambao Bwana aliufanya na Ibrahimu na uzao wake.

Vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale viliandikwa na Musa. Navyo ni Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati. Mwanzo kinaelezea asili ya dunia, mwanadamu, lugha, jamii, na mwanzo wa nyumba ya Israeli.

Vitabu hivi vya kihistoria vinasimulia juu ya matukio ya Israeli. Vitabu hivyo ni Yoshua, Waamuzi, Rutu, 1 na 2 Samweli, 1 na 2 Wafalme, 1 na 2 Mambo ya Nyakati, Ezra, Nehemia, na Esta.

Vitabu vya kishairi vinaandika baadhi ya hekima na ustadi wa lugha wa manabii. Navyo ni Ayubu, Zaburi, Mithali, Mhubiri, Wimbo wa Suleimani, na Maombolezo.

Manabii walimwonya Israeli juu ya dhambi zake na wakatoa ushuhuda juu ya baraka zinazokuja kutokana na utii. Walitoa unabii juu ya kuja kwa Kristo, ambaye angelipia dhambi za wale ambao wanatubu, kupokea ibada, na kuishi kulingana na injili. Vitabu vya manabii ni Isaya, Yeremia, Ezekieli, Danieli, Hosea, Yoeli, Amosi, Obadia, Yona, Mika, Nahumu, Habakuki, Zefania, Hagai, Zekaria, na Malaki.

Vitabu vingi vya Agano la Kale viliandikwa katika Kiebrania. Maandishi machache yalikuwa ya Kiaramaya, lugha inayofanana na Kiebrania.