Misaada ya Kujifunza
Mauti ya Kiroho


Mauti ya Kiroho

Kutengwa na Mungu na nguvu Zake; ni kufa kwa mambo yahusuyo haki. Lusiferi na theluthi moja ya majeshi ya mbinguni walikubali mauti ya kiroho wakati walipotupwa kutoka mbinguni (M&M 29:36–37).

Mauti ya kiroho yaliletwa ulimwenguni kwa Anguko la Adamu (Musa 6:48). Wenye mwili wenye kufa na mawazo, maneno, na matendo maovu wamekufa kiroho wakati wangali hai hapa duniani (1 Tim. 5:6). Kwa Upatanisho wa Yesu Kristo na kwa kutii kanuni na ibada za injili, wanaume na wanawake wanaweza kuwa safi kwa kutoka katika dhambi na kushinda mauti ya kiroho.

Mauti ya kiroho pia hutokea kufuatia kifo cha mwili wenye kufa. Viumbe wafufuka na ibilisi na malaika zake wote watahukumiwa. Wale wote walioasi kwa makusudi dhidi ya nuru na kweli ya injili watateseka mauti ya kiroho. Kifo hiki mara nyingi huitwa kifo cha pili (Alma 12:16; Hel. 14:16–19; M&M 76:36–38).