Misaada ya Kujifunza
Herode


Herode

Ni jamaa ya watawala katika Yuda iliyokuwepo karibu na wakati wa Yesu Kristo. Walikuwa ni watu muhimu katika matukio mengi ya Agano Jipya. Familia hii ilianzishwa na Herode Mkuu, ambaye alikuwa mwoga kwa kuzaliwa kwa Mwokozi (Mt. 2:3) na akatoa agizo la mauaji ya kimbari ya watoto wachanga katika Bethlehemu. Wanawe wa kiume ni pamoja na Aristobulo; Herode Filipo (Mt. 14:3; Mk. 6:17); Herode Antipasi, mfalme (Mt. 14:1; Lk. 9:7; pia ialijulikana kama Mfalme Herode, Mk. 6:14); Arkelao (Mt. 2:22); na Filipo, mfalme wa Iturea (Lk. 3:1). Herod Agrippa Ⅰ (Mdo. 12:1–23) na dada yake Herodia (Mt. 14:3; Mk. 6:17) walikuwa watoto wa Aristobulo. Herode Agrippa Ⅰ pia alikuwa na watoto kadhaa ambao wametajwa katika Agano Jipya, akijumuishwa na Herod Agrippa Ⅱ (Mdo. 25:13), Bernike (Mdo. 25:13), na Drusila, mke wa Feliki (Mdo. 24:24).