Kama linavyotumika katika maandiko, familia ndani yake kuna mume na mke, watoto, na wakati mwingine jamaa wengine wanaoishi katika nyumba moja au chini ya kiongozi mmoja wa familia. Familia pia yaweza kuwa ya mzazi mmoja pamoja na watoto, mume na mke bila watoto, au hata mtu mmoja aishiye peke yake.
Katika wewe jamaa zote za duniani zitabarikiwa, Mwa. 12:3 (Mwa. 28:14 ; Ibr. 2:11 ).
Nitakuwa Mungu wa familia zote za Israeli, Yer. 31:1 .
Utukufu wako utakuwa kuendelea kwa uzao wako milele, M&M 132:19 .
Nitampa taji la uzawa wa milele katika dunia za milele, M&M 132:55 .
Kufunganishwa kwa watoto kwa wazazi ni sehemu ya kazi kuu ya utimilifu wa nyakati, M&M 138:48 .
Mwana mume na mwanamke niliwaumba, na nikawaambia: Zaeni na mkaongezeke, Musa 2:27–28 .
Si vyema kwa mtu huyo kuwa pekee yake, Musa 3:18 .
Adamu na Hawa walifanya kazi pamoja, Musa 5:1 .
Ibrahimu atawaamuru watoto wake, nao wataishika njia ya Bwana, Mwa. 18:17–19 .
Nawe uwafundishe watoto wako maneno haya kwa bidii, Kum. 6:7 (Kum. 11:19 ).
Yeye ampendaye mwanawe humrudi, Mit. 13:24 (Mit. 23:13 ).
Mlee mtoto katika njia impasayo, Mit. 22:6 .
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, Mh. 9:9 .
Watoto wako watafundishwa na Bwana, Isa. 54:13 (3Â Ne. 22:13 ).
Waleeni katika malezi ya Bwana, Efe. 6:1–4 (Eno. 1:1 ).
Kama mtu yeyote hawatunzi walio wake, ameikana imani, 1Â Tim. 5:8 .
Aliwasihi kwa huruma zote za mzazi mwenye upendo, 1Â Ne. 8:37 .
Tunazungumza juu ya Kristo ili watoto wetu wapate kujua chanzo kipi wapate kukitazamia, 2Â Ne. 25:26 .
Waume zao na wake zao wanawapenda watoto wao, Yak. (KM) 3:7 .
Wafundisheni kupendana na kutumikiana, Mos. 4:14–15 .
Mtazilinda familia zenu hata kwa kumwaga damu, Alma 43:47 .
Salini katika familia zenu ili wake zenu na watoto wenu wapate kubarikiwa, 3Â Ne. 18:21 .
Wazazi watafundisha injili kwa watoto wao, M&M 68:25 .
Kila mtu analazimika kutunza familia yake yeye mwenyewe, M&M 75:28 .
Watoto wote wanayo haki ya madai juu ya wazazi wao, M&M 83:4 .
Waleeni watoto wenu katika nuru na kweli, M&M 93:40 .
Iweke sawa nyumba yako wewe mwenyewe, M&M 93:43–44, 50 .
Makuhani yawapasa tu kuwashawishi wengine kwa upendo usio na unafiki, M&M 121:41 .
Waheshimu baba yako na mama yako, Ku. 20:12 .
Mwanangu, sikiliza mafundisho ya baba yako, Mit. 1:8 (Mit. 13:1 ; 23:22 ).
Yesu alikuwa chini ya wazazi wake, Lk. 2:51 .
Yesu alifanya mapenzi ya baba yake, Yn. 6:38 (3Â Ne. 27:13 ).
Watiini wazazi wenu katika Bwana, Efe. 6:1 (Kol. 3:20 ).
Mafundisho na Maagano yanaelezea asili ya umilele wa uhusiano wa ndoa na familia. Ndoa ya selestia na uendelezo wa familia unawawezesha waume na wake kuwa miungu (M&M 132:15–20 ).