Kaburi Ona pia Ufufuko Mahali pa kuzika mwili ufao. Kwa sababu ya Upatanisho, kila mtu atafufuka kutoka kaburini. Baada ya ufufuko wa Kristo, makaburi yakafunuka na miili mingi ikainuka, Mt. 27:52–53 (3 Ne. 23:9–13). Ewe kaburi, u wapi ushindi wako, 1 Kor. 15:55. Kaburi ni lazima liwatoe wafu wake, 2 Ne. 9:11–13. Wale waliolala kaburini watatoka, M&M 88:97–98. Kisima cha ubatizo ni ishara ya kaburi, M&M 128:12–13.