Upungufu au ukosefu wa unyenyekevu au kutofundishika. Kiburi huwaweka watu katika upinzani wao kwa wao na kwa Mungu. Mtu mwenye majivuno hujiweka yeye mwenyewe juu ya wale wanaomzunguka na hufuata mapenzi yake zaidi kuliko mapenzi ya Mungu. Makuu, husuda, ugumu wa moyo, na maringo pia ni tabia za mtu mwenye majivuno.
Jihadhari kwamba usije ukamsahau Bwana na moyo wako ukainuka, Kum. 8:11–14 .
Kiburi na majivuno navichukia, Mit. 8:13 (Mit. 6:16–17 ).
Kiburi hutangulia uangamivu, Mit. 16:18 .
Siku ya Bwana itakuwa juu ya wenye kiburi, Isa. 2:11–12 (2 Ne. 12:11–12 ).
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Oba. 1:3 .
Wote wenye kiburi watakuwa makapi, Mal. 4:1 (1Â Ne. 22:15 ; 3Â Ne. 25:1 ; M&M 29:9 ).
Yeyote atakayejikweza, atadhiliwa, Mt. 23:12 (M&M 101:42 ).
Mungu huwapinga wenye kiburi, 1Â Pet. 5:5 .
Lile jengo kuu na pana lilikuwa ni kiburi cha ulimwengu, 1Â Ne. 11:36 (1Â Ne. 12:18 ).
Wanapoelimika wanadhani kwamba wana hekima, 2 Ne. 9:28–29 .
Mmejiinua katika kiburi cha mioyo yenu, Yak. (KM) 2:13, 16 (Alma 4:8–12 ).
Mmevuliwa kiburi, Alma 5:28 .
Kiburi kikubwa kupita kiasi kimeingia katika mioyo ya watu, Hel. 3:33–36 .
Je, ni haraka ya jinsi gani watoto wa watu huinuliwa katika kiburi? Hel. 12:4–5 .
Kiburi cha taifa hili kinathibitisha angamizo lao, Moro. 8:27 .
Jihadharini na kiburi, msije mkawa kama Wanefi, M&M 38:39 .
Acheni kiburi na upuuzi wenu wote, M&M 88:121 .