Misaada ya Kujifunza
Mizeituni, Mlima wa


Mizeituni, Mlima wa

Kilima kilicho katika mashariki ya Bonde la Kidroni, mashariki ya Yerusalemu. Juu ya miteremko yake ya magharibi, karibu na chini, ndipo ilipo bustani ya Gethsemani. Bethfage na Bethania zipo juu yake na katika mteremko wa mashariki. Mlima huu ulikuwa mahali pa matukio mengi ya kibiblia (Mt. 24:3) na pia patakuwa mahali muhimu katika matukio ya siku za mwisho (Zek. 14:3–5; M&M 45:48–54; 133:20).