Misaada ya Kujifunza
Hagai


Hagai

Nabii wa Agano la Kale ambaye alitoa unabii katika karibu mwaka 520 K.K. katika Yerusalemu, mara baada ya watu wa Uyahudi waliporudi kutoka katika uhamisho wa Babilonia (Ezra 5:1; 6:14). Alisema juu ya kujengwa hekalu la Bwana katika Yerusalemu na akawakemea watu kwa sababu hawakuwa wamemaliza. Naye pia aliandika juu ya hekalu la milenia na utawala wa Mwokozi.

Kitabu cha Hagai

Katika mlango wa 1, Bwana anawakemea watu kwa kuishi katika nyumba zao zilizomalizika wakati hekalu limebaki bila kujengwa. Mlango wa 2 unaandikwa unabii wa Hagai kwamba Bwana atatoa amani katika hekalu Lake.