Misaada ya Kujifunza
Yakobo, Mwana wa Lehi


Yakobo, Mwana wa Lehi

Nabii katika Kitabu cha Mormoni na mtunzi wa mahubiri kadhaa katika vitabu vya 2 Nefi na Yakobo (2 Ne. 6–11; Yak. [KM] 1–7).

Kitabu cha Yakobo

Kitabu cha tatu katika kitabu cha Mormoni. Mlango wa 1 hutuambia kwamba Nefi alimkabidhi Yakobo kumbukumbu iliyoandikwa na kisha akamweka wakfu Yakobo na kaka yake Yusufu ili wawe makuhani na walimu kwa watu. Mlango wa 2–4 ni mahubiri yanayowasisitizia watu kuwa safi kimaadili. Yakobo pia alifundisha juu ya ujio wa Masiya mkombozi, na akatoa sababu kwa nini baadhi katika Israeli wasingemkubali wakati wa ujio Wake. Mlango wa 5–6 ina ushuhuda wa Yakobo na fumbo la kinabii juu ya historia na misheni ya watu wa Israeli. Mlango wa 7 una historia ya mwasi msomi aliyeitwa Sheremu, ambaye alishindwa kwa ushuhuda mtakatifu wa Yakobo.