Misaada ya Kujifunza
Kiapo na Agano la Ukuhani


Kiapo na Agano la Ukuhani

Kiapo ni uthibitisho ulioapwa kuwa mtu atakuwa mkweli na mwaminifu katika ahadi zake. Agano ni ahadi ya dhati kati ya pande mbili. Ukuhani wa Haruni hupokelewa kwa agano peke yake. Wenye Ukuhani wa Melkizedeki hupokea ukuhani kwa kiapo na kwa agano lisilotamkwa. Kama wenye ukuhani watakuwa waaminifu na wenye kuikuza miito yao kama Mungu anavyoelekeza, Yeye huwabariki. Wale wanao kuwa waaminifu hadi mwisho na watendao yote Anayo waagiza kufanya watapata yale yote Baba aliyo nayo (M&M 84:33–39).