Msaada wa Masomo
Mwongofu, Uongofu
iliyopita inayofuata

Mwongofu, Uongofu

Mtu kubadili imani, moyo, na maisha kwa kukubali na kufuata mapenzi ya Mungu (Mdo. 3:19).

Uongofu unajumuisha uamuzi wa makusudi wa mtu kuacha njia zake za zamani na kubadilika na kuwa mfuasi wa Kristo. Toba, ubatizo kwa ajili ya ondoleo la dhambi, mapokezi ya Roho Mtakatifu kwa kuwekewa juu mikono, na imani endelevu kwa Bwana Yesu Kristo hufanya uongofu uwe mkamilifu. Mtu wa asili atabadilika na kuwa mtu mpya aliyetakaswa na aliye safi, aliyezaliwa tena katika Kristo Yesu (2 Kor. 5:17; Mos. 3:19).