Misaada ya Kujifunza
Sinagogi


Sinagogi

Mahali pa kukutania palipotumika kwa madhumuni ya kidini. Katika nyakati za Agano Jipya, samani zake kwa ujumla zilikuwa za kawaida, zikiwa ni sanduku lenye hati ndefu za kukunja za torati na maandishi mengine matakatifu, meza ya kusomea, na viti kwa ajili ya wenye kuabudu.

Baraza la wazee wenyeji wa eneo walisimamia kila sinagogi. Wao ndiyo walioamua nani aruhusiwe kuingia na nani atengwe (Yn. 9:22; 12:42). Ofisa muhimu zaidi alikuwa ni yule mtawala wa sinagogi hiyo (Mk. 5:22; Lk. 13:14). Kwa ujumla yeye alikuwa mwandishi, alikuwa mtunzaji wa jengo hilo, na alisimamia ibada hizo. Mhudumu alikuwa akitenda kazi za kiukarani (Lk. 4:20).

Palikuwepo sinagogi katika kila mji ambao Wayahudi walikuwa wakiishi, kote katika Palestina na kwingineko kote. Huu ulikuwa ni msaada mkubwa katika kueneza injili ya Yesu Kristo kwa sababu wamisionari wa kwanza wa Kanisa kwa kawaida waliweza kuzungumza katika masinagogi haya (Mdo. 13:5, 14; 14:1; 17:1, 10; 18:4). Desturi hii ilikuwepo miongoni mwa wamisionari katika Kitabu cha Mormoni (Alma 16:13; 21:4–5; 32:1), vile vile miongoni mwa wamisionari wa mwanzoni katika kipindi hiki (M&M 66:7; 68:1).