Misaada ya Kujifunza
Samaria


Samaria

Katika Agano la Kale, ni mji mkuu wa ufalme wa kaskazini wa Israeli (1 Fal. 16:23–24). Kwa sababu ya nafasi yake ya uimara wa kijeshi juu ya mlima, Waashuru hawakuweza kuuteka hadi baada ya kuuhusuru kwa miaka mitatu (2 Fal. 17:5–6). Herodi aliujenga upya na akauita Sebaste. Katika nyakati za Agano Jipya, Samaria lilikuwa ndilo jina la sehemu yote ya katikati ya Palestina magharibi ya Yordani.