Misaada ya Kujifunza
Agano Jipya


Agano Jipya

Mkusanyiko wa maandishi yaliyoandikwa kwa kuongozwa na Mungu (mwanzoni yalikuwa ya Kiyunani) juu ya maisha na huduma ya Yesu Kristo, Mitume, na wanafunzi wengine wa Yesu Kristo. Agano Jipya kwa ujumla limegawanyika katika Injili, Matendo ya Mitume, nyaraka za Paulo, nyaraka za jumla, na kitabu cha Ufunuo.

Injili nne—vitabu vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana—ni taarifa juu ya maisha ya Kristo. Kitabu cha Matendo kinaandika historia ya Kanisa na Mitume, hususani safari za Paulo za kimisionari, baada ya kifo cha Kristo. Barua za Paulo hutoa mafundisho kwa viongozi wa Kanisa na waumini. Barua nyingine ziliandikwa na Mitume wengine nazo zinatoa nyongeza ya ushauri kwa Watakatifu wa awali. Kitabu cha Ufunuo, ambacho kiliandikwa na Mtume Yohana kina unabii zaidi uhusuo siku za mwisho.