Misaada ya Kujifunza
Luka


Luka

Mwandishi wa Injili ya Luka na kitabu cha Matendo katika Agano Jipya na mmisionari mwenza wa Paulo. Alizaliwa kwa wazazi wa Kiyunani na alikuwa tabibu (Kol. 4:14). Luka alikuwa msomi mzuri. Alijitambulisha mwenyewe kama mwenza wa Mtume Paulo wakati alipoungana na Paulo huko Troasi (Mdo. 16:10–11). Luka alikuwa pia pamoja na Paulo huko Filipi katika safari ya mwisho ya Paulo ya kwenda Yerusalemu (Mdo. 20:6), nao wawili walikuwa pamoja hadi walipowasili Roma. Luka alikuwa pia pamoja na Paulo wakati wa kifungo chake cha pili gerezani huko Roma (2 Tim. 4:11). Mapokeo yanasema alikufa kifo cha kishahidi.

Injili ya Luka

Taarifa ambayo Luka aliiandika juu ya Yesu Kristo na huduma Yake alipokuwa katika mwili wenye kufa. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni endelezo la Injili ya Luka. Luka aliacha taarifa iliyoandikwa vyema juu ya huduma ya Yesu, akimwelezea Yesu kama Mwokozi wa wote Wayahudi na Wayunani. Aliandika mengi juu ya mafundisho ya Yesu na matendo Yake. Katika Luka tunapata tu habari za Gabrieli kuwatembelea Zakaria na Maria (Lk. 1); matembezi ya wachunga kondoo kwa mtoto Yesu (Lk. 2:8–18); Yesu hekaluni akiwa na umri wa miaka kumi na miwili (Lk. 2:41–52); kuamriwa na kutumwa kwa wale sabini (Lk. 10:1–24). Yesu anatoka jasho la damu (Lk. 22:44); majadiliano ya Yesu na mwizi juu ya msalaba (Lk. 23:39–43); na Yesu anakula samaki na asali baada ya Ufufuko Wake (Lk. 24:42–43).

Kwa orodha ya matukio katika maisha ya Mwokozi yaliyoelezwa katika Injili ya Luka, ona Upatanifu wa Injili katika kiambatisho.