Dada Ona pia Kaka, Ndugu; Mwanadamu, Wanadamu; Mwanamke, Wanawake Kama watoto wa baba yetu wa Mbinguni, wanaume na wanawake wote ni kaka na dada wa kiroho. Katika Kanisa, waumini wanawake na marafiki wa Kanisa mara kwa mara hutambulika kama dada. Wale wafanyao mapenzi ya Baba yangu, hao ndiyo kaka na dada yangu, Mt. 12:50 (Mk. 3:35). Sheria zinazotawala maungamo ya dhambi kati ya kaka na dada katika Kanisa zinawekwa, M&M 42:88–93.