Nira Ona pia Mwanafunzi Chombo kinachovikwa kuzunguka shingo ya wanyama au watu ili kufungwa pamoja. Nira ya Kristo ni ishara ya uanafunzi, wakati nira ya utumwa ni ishara ya ukandamizaji. Nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi, Mt. 11:29–30. Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, 2 Kor. 6:14. Msinaswe kwa nira ya utumwa, Gal. 5:1. Wala hatutamani kumleta yoyote kwenye nira ya utumwa, Alma 44:2. Mateso ya Watakatifu ni nira ya chuma, kamba imara, na minyororo ya jehanamu, M&M 123:1–3, 7–8.