Misaada ya Kujifunza
Harris, Martin


Harris, Martin

Mmoja wa Mashahidi Watatu wa asili ya utakatifu na wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Alimsaidia kifedha Joseph Smith na Kanisa. Bwana alimwambia Martin Harris auze shamba lake na kutoa fedha hizo ili kulipia uchapishaji wa Kitabu cha Mormoni (M&M 19:26–27, 34–35), ili awe mfano kwa Kanisa (M&M 58:35), na ili kusaidia kulipia gharama za huduma (M&M 104:26).

Martin Harris alitengwa na Kanisa lakini baadaye alirejea na kuwa muumini kamili. Hadi mwisho wa maisha yake aliendelea kutoa ushahidi kwamba alimwona malaika Moroni na yale mabamba ya dhahabu ambayo kutoka hayo Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni.