Misaada ya Kujifunza
Siku ya Sabato


Siku ya Sabato

Siku takatifu iliyotengwa kila wiki kwa ajili ya kupumzika na kuabudu. Baada ya Mungu kuumba vitu vyote, Alipumzika siku ya saba na akaamuru kwamba siku moja katika kila wiki iwe siku ya kupumzika ili kuwasaidia watu kumkumbuka Yeye (Ku. 20:8–11).

Kabla ya kufufuka kwa Yesu Kristo, waumini wa Kanisa waliiheshimu siku ya mwisho ya wiki kama Sabato, kama walivyofanya Wayahudi. Baada ya Ufufuko, waumini wa Kanisa, wawe Wayahudi au Wayunani, waliiheshimu siku ya kwanza ya wiki (ile siku ya Bwana) ili kukumbuka Ufufuko wa Bwana. Kanisa siku hizi huendelea kuheshimu siku moja ya wiki kama siku takatifu ya Sabato ambapo siku hiyo humuabudu Mungu na kupumzika kutokana na kazi za ulimwengu.

Sabato huwakumbusha watu juu ya umuhimu wao wa chakula cha kiroho na wajibu wao wa kumtii Mungu. Wakati taifa linapokuwa halijali katika kutii Sabato, hali zote za maisha huathirika na maisha yake ya kidini huoza (Neh. 13:15–18; Yer. 17:21–27).