Maandiko Matakatifu
Ibrahimu 5


Mlango wa 5

Miungu wanamaliza mipango Yao ya uumbaji wa vitu vyote—Wanatimiza Uumbaji kulingana na mipango Yao—Adamu atoa majina kwa kila kiumbe hai.

1 Na hivyo ndivyo tutakavyomaliza mbingu na dunia, na majeshi yao yote.

2 Na Miungu wakasemezana miongoni mwao: Na mara ya asaba tutamaliza kazi yetu, ambayo tumekubaliana; nasi tutapumzika ifikapo mara ya saba kutokana na kazi zetu zote ambazo tumekubaliana kuzifanya.

3 Na Miungu wakahitimisha ilipofika mara ya saba, kwa sababu ifikapo mara ya saba awatapumzika kutokana na kazi zao zote ambazo wao (Miungu) walikubaliana wao wenyewe kuzifanya; na bwakaitakasa. Na huo ndiyo ulikuwa uamuzi wao wakati walipokubaliana miongoni mwao wenyewe kuzifanya mbingu na dunia.

4 Na Miungu wakashuka na kuvifanya hivi vizazi vya mbingu na dunia, wakati vilipofanywa katika siku ile Miungu walipozifanya dunia na mbingu,

5 Kulingana na yale yote waliyoyasema juu ya kila mmea wa kondeni akabla haujakuwepo duniani, na kila mche wa kondeni kabla ya kuota; kwa maana Miungu walikuwa hawajaifanya mvua kunyesha juu ya dunia wakati waliposhauriana kuvifanya, na walikuwa hawajafanya mtu wa kuilima ardhi.

6 Lakini ukapanda ukungu katika dunia, na ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

7 Na aMiungu wakamfanya mtu kutokana na bmavumbi ya ardhi, na wakaichukua croho yake (yaani, roho ya mtu yule), na kuiweka ndani yake; na wakaipulizia katika pua zake pumzi ya uhai, naye mtu akawa dnafsi hai.

8 Nao Miungu wakapanda bustani, nayo aEdeni ilikuwa katika upande wa mashariki, na hapo wakamweka mtu, ambaye roho yake waliiweka ndani ya mwili ambao waliutengeneza.

9 Na kutoka ardhini Miungu wakafanya kila mti uote ulio wenye kupendeza machoni na mwema kwa chakula; amti wa uzima, pia, katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na maovu.

10 Palikuwepo na mto kutoka Edeni, wa kumwagilia maji bustani, na kutoka hapo uligawanyika na kuwa na vichwa vinne.

11 Na Miungu wakamchukua yule mtu na kumweka katika Bustani ya Edeni, ili ailime na kuitunza.

12 Na wale Miungu wakamwamuru yule mtu, wakisema: Matunda ya kila mti wa bustani uko huru kuyala,

13 Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na maovu, usile; kwa maana wakati utakapoyala matunda yake, hakika utakufa. Sasa mimi, Ibrahimu, niliona ya kwamba ilikuwa kwa jinsi ya awakati wa Bwana, ambao ulikuwa kwa jinsi ya wakati wa bKolobu; kwa kuwa ilikuwa bado Miungu hawajampangia Adamu kuhesabu kwake.

14 Na Miungu wakasema: Na tuumbe msaidizi wa kumfaa mtu huyu, kwa maana siyo vyema mtu huyu kuwa peke yake, kwa hiyo tutamuumbia msaidizi wa kumfaa.

15 Na Miungu wakafanya usingizi mzito ukaja juu ya aAdamu; naye akalala, nao wakachukua ubavu wake mmoja, na wakafunika kwa nyama mahali pake;

16 Na ule ubavu ambao Miungu waliuchukua kutoka kwa yule mtu, wakamfanya amwanamke, na wakamleta kwa mtu yule.

17 Na Adamu akasema: Huyu alikuwa mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama yangu; sasa ataitwa Mwanamke, kwa sababu yeye alitwaliwa kutoka kwa mwanaume;

18 Kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye aataambatana na mke wake, nao watakuwa mwili bmmoja.

19 Nao wote walikuwa uchi, mtu na mke wake, na wala hawakuona aibu.

20 Na kutokana na ardhi Miungu wakaumba kila mnyama wa kondeni, na kila ndege wa angani, na wakawaleta kwa Adamu ili waone atawaitaje; na lolote Adamu aliloliita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.

21 Na Adamu akatoa majina kwa wanyama wote wafugwao, kwa ndege wa angani, kwa kila mnyama wa mwituni; na kwa Adamu, alipatikana msaidizi wa kumfaa.