Misaada ya Kujifunza
Roho


Roho

Ile sehemu ya kiumbe hai ambayo ilikuwepo kabla ya kuzaliwa duniani, ile ikaayo ndani ya mwili wa nyama na mifupa wakati wa maisha katika mwili wenye kufa, na itakuwepo baada ya kifo kama kiumbe kinachojitegemea hadi ufufuko. Vitu vyote vyenye uhai—mwanadamu, wanyama, na mimea—vilikuwa roho kabla ya uhai haujakuwepo juu ya dunia (Mwa. 2:4–5; Musa 3:4–7). Mwili wa roho huonekana kama mwili wa kawaida (1 Ne. 11:11; Eth. 3:15–16; M&M 77:2; 129). Roho ni maada, lakini ni angavu zaidi au safi kuliko kitu cha asili cha duniani au maada (M&M 131:7).

Kila mtu ni mwana au binti halisi wa Mungu, akiwa amezaliwa kama roho kwa Wazazi wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa kwa wazazi wenye mwili wenye kufa duniani (Ebr. 12:9). Kila mtu duniani anao mwili usiokufa wa kiroho kama nyongeza kwa mwili wa nyama na mifupa. Kama wakati mwingine ilivyofafanuliwa katika maandiko, roho na mwili wa kawaida kwa pamoja hufanya nafsi (Mwa. 2:7; M&M 88:15; Musa 3:7, 9, 19; Ibr. 5:7). Roho inaweza kuishi pasipo mwili, lakini mwili hauwezi kuishi pasipo roho (Yak. [Bib.] 2:26). Kifo cha kimwili ni kujitenga kwa roho kutoka katika mwili. Katika Ufufuko, roho inaungana tena na mwili ule ule wa nyama na mifupa iliokuwa ikiumiliki kama mtu mwenye kufa, ukiwa na tofauti kubwa mbili: havitatengana tena, na ule mwili utakuwa mwili usiokufa na mkamilifu (Alma 11:45; M&M 138:16–17).

Pepo wachafu