Misaada ya Kujifunza
Betheli


Betheli

Katika Kiebrania, maana yake “nyumba ya Mungu” na ni moja ya maeneo matakatifu sana katika Israeli. Uko kiasi maili kumi (kilometa kumi na sita) kaskazini mwa Yerusalemu. Hapa Ibrahimu alijenga madhabahu yake alipofika Kanaani kwa mara ya kwanza (Mwa. 12:8; 13:3). Hapa Yakobo aliona katika ono ngazi ifikayo mbinguni (Mwa. 28:10–19). Pia palikuwa mahali patakatifu katika siku za Samweli (1 Sam. 7:16; 10:3).