Misaada ya Kujifunza
Ono la Kwanza


Ono la Kwanza

Kutokea kwa Mungu Baba na Mwanawe Yesu Kristo kwa Joseph Smith Nabii katika kijisitu cha miti.

Katika majira ya kuchipua ya mwaka 1820, Joseph Smith Mdogo, alikuwa katika mwaka wake wa kumi na nne. Yeye alikuwa akiishi na familia yake katika eneo la Palmyra, New York. Umbali mfupi magharibi mwa nyumba ya familia hiyo kilikuwepo kijisitu cha miti mikubwa. Joseph alikwenda mahali hapa kusali kwa Mungu ili kujua kanisa lipi lilikuwa la kweli. Alikuwa amevutiwa wakati akisoma Biblia kwamba alilazimika kuomba jibu kutoka kwa Mungu (Yak. [Bib.] 1:5–6). Katika jibu la sala yake, Baba na Mwana wakamtokea yeye na kumwambia asijiunge na lolote kati ya makanisa hayo yaliyokuwepo duniani, kwani yote hayakuwa sahihi uongo (JS—H 1:15–20). Tukio hili takatifu lilianzisha mfuatano wa matukio ambayo yangeleta Urejesho wa injili na Kanisa la kweli la Kristo.