Yesu Kristo ndiye Mkombozi mkuu wa wanadamu kwa sababu Yeye, kupitia Upatanisho Wake, alilipia dhambi za wanadamu na akawezesha kupatikana kwa ufufuko wa watu wote.
Ninajua kwamba mkombozi wangu yu hai, Ayu. 19:25 .
Nitakusaidia, asema mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, Isa. 41:14 (Isa. 43:14 ; 48:17 ; 54:5 ; 59:20 ).
Mimi Bwana ndiye Mkombozi wako, Isa. 49:26 (Isa. 60:16 ).
Mtamwita jina lake Yesu: kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao, Mt. 1:21 .
Mwana wa Mtu amekuja kuutoa uhai wake kama fidia kwa ajili ya wengi, Mt. 20:28 (1 Tim. 2:5–6 ).
Bwana Mungu wa Israeli amewatembele na kuwakomboa watu wake, Lk. 1:68 .
Tulipatanishwa kwa Mungu kwa kifo cha Mwanawe, Rum. 5:10 .
Yesu Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu, ili apate kutukomboa na uovu wote, Tit. 2:13–14 .
Yesu Kristo alituosha dhambi zetu katika damu yake yeye mwenyewe, Ufu. 1:5 .
Ukombozi huja katika na kupitia Masiya Mtakatifu, 2 Ne. 2:6–7, 26 .
Mwana alijitwalia juu yake uovu na uvunjaji sheria wa wanadamu, akawakomboa, na akatosheleza madai ya haki, Mos. 15:6–9, 18–27 .
Kristo alikuja kuwakomboa wale wote ambao wangebatizwa ubatizo wa toba, Alma 9:26–27 .
Atakuja ulimwenguni kuwakomboa watu wake, Alma 11:40–41 .
Ukombozi huja kwa njia ya toba, Alma 42:13–26 .
Yesu alikuja kuukomboa ulimwengu, Hel. 5:9–12 .
Kristo amewakomboa wanadamu kutokana na kifo cha kimwili na kiroho, Hel. 14:12–17 .
Ukombozi huja kupitia kwa Kristo, 3Â Ne. 9:17 .
Mimi ndiye niliyetayarishwa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu ili kuwakomboa watu wangu, Eth. 3:14 .
Bwana Mkombozi wenu aliteseka mauti katika mwili, M&M 18:11 .
Kristo aliteseka kwa ajili ya wote kama watatubu, M&M 19:1, 16–20 .
Watoto wadogo wamekombolewa kupitia Mwana wa Pekee, M&M 29:46 .
Nimempeleka Mwanangu wa Pekee katika ulimwengu kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu, M&M 49:5 .
Kristo ndiye nuru na Mkombozi wa ulimwengu, M&M 93:8–9 .
Joseph F. Smith alipokea ono juu ya wokovu wa wafu, M&M 138 .