Misaada ya Kujifunza
Ashuru


Ashuru

Ufalme wa kale ambao, pamoja na mpinzani wake Babiloni, walitawala sehemu kubwa ya mataifa ya zamani ya Shamu na Palestina karibu kipindi chote cha nyakati za Agano la Kale. Ingawa Waashuru walikuwa na nguvu kubwa katikati ya karne ya 12 K.K. hadi karibu mwishoni mwa karne ya 7 K.K., kamwe hawakuweza kujenga muundo imara wa kisiasa. Walitawala kwa vitisho, wakiwasaga maadui zao kwa moto na upanga au kwa kuwadhoofisha kwa kuwahamisha sehemu kubwa ya idadi ya watu kwenda sehemu nyingine ya ufalme wao. Watu wale ambao waliwekwa chini ya utawala wa Washuru mara kwa mara walipigana dhidi ya ile milki. (Ona 2 Fal. 18–19; 2 Nya. 32; Isa. 7:17–20; 10; 19; 37.)