Misaada ya Kujifunza
Nahumu


Nahumu

Nabii wa Agano la Kale wa Galilaya aliyeandika unabii wake wakati fulani kati ya mwaka 642 na 606 K.K.

Kitabu cha Nahumu

Mlango wa 1 huzungumzia juu ya kuunguzwa kwa dunia wakati wa Ujio wa Pili na juu ya huruma na uwezo wa Bwana. Mlango wa 2 huelezea juu ya angamizo la Ninawi, ambalo ni kivuli cha kile kitakachokuja katika siku za mwisho. Mlango wa 3 unaendelea kutaja angamizo la kuhuzunisha la Ninawi.