Misaada ya Kujifunza
Maandiko


Maandiko

Maneno, yaliyoandikwa na kusemwa, na watu watakatifu wa Mungu wakiwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu. Maandiko matakatifu yanayotambuliwa rasmi na Kanisa siku hizi ni pamoja na Biblia, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu. Yesu na waandishi wa Agano Jipya waliviheshimu vitabu vya Agano Jipya kama maandiko (Mt. 22:29; Yn. 5:39; 2 Tim. 3:15; 2 Pet. 1:20–21). Ona pia Wendo katika kiambatisho.

Maandiko yaliyopotea

Kuna maandishi mengi matakatifu yaliyotajwa katika maandiko ambayo hatunayo leo, miongoni mwake ni vitabu hivi na waandishi hawa: agano (Ku. 24:7), vita vya Bwana (Hes. 21:14); Yashari (Yos. 10:13; 2 Sam. 1:18), matendo ya Sulemani (1 Fal. 11:41), Samweli mwonaji (1 Nya. 29:29), Nathali nabii (2 Nya. 9:29), Shemaya nabii (2 Nya. 12:15), Ido nabii (2 Nya. 13:22), Yehu (2 Nya. 20:34), misemo ya waonaji (2 Nya. 33:19), Henoko (Yuda 1:14), na maneno ya Zenoki, Neumu, na Zeno (1 Ne. 19:10), Zeno (Yak. [KM] 5:1), Zenoki na Ezia (Hel. 8:20), na kitabu cha ukumbusho (Musa 6:5); na nyaraka kwa Wakorintho (1 Kor. 5:9), kwa Waefeso (Efe. 3:3), na kutoka Laodikia (Kol. 4:16), na kutoka Yuda (Yuda 1:3).

Maandiko yahifadhiwe

Thamani ya maandiko

Maandiko yaliyotolewa unabii kwamba yatakuja