Ukengeufu Ona pia Uasi; Urejesho wa Injili Kugeuka mbali na ukweli kwa mtu binafsi, Kanisa, au taifa lote. Ukengeufu wa jumla Israeli walijilinda mioyo yao isigeuke mbali na Bwana, Kum. 29:18. Pale pasipo maono, watu huangamia, Mit. 29:18. Wamelivunja agano lisilo na mwisho, Isa. 24:5. Pepo zikapiga nyumba ile, nayo ikaanguka, Mt. 7:27. Nastaajabu kwamba kwa upesi mmegeukia katika injili nyingine, Gal. 1:6. Walianza katika njia nzuri lakini katikati ya ukungu wakaipoteza njia yao, 1 Ne. 8:23 (1 Ne. 12:17). Baada ya kuonja lile tunda, wakaangukia katika njia zilizokatazwa, 1 Ne. 8:28. Ukengeufu wa Wanefi ulisababisha vikwazo kwa wale wasio amini, Alma 4:6–12. Waumini wengi wa Kanisa wakawa na kiburi na wakiwatesa waumini wengine, Hel. 3:33–34 (Hel. 4:11–13; 5:2–3). Bwana anapowastawisha watu wake nyakati nyingine wao hushupaza mioyo yao na kumsahau yeye, Hel. 12:2; 13:38. Wanefi walishupaza mioyo yao na kuanguka chini ya uwezo wa Shetani, 3 Ne. 2:1–3. Moroni alitoa unabii juu ya uasi katika siku za mwisho, Morm. 8:28, 31–41. Ukengeufu utatangulia Ujio wa Pili, M&M 1:13–16. Ukengeufu wa Kanisa la awali la Kikristo Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao, Isa. 29:10, 13. Giza litaifunika dunia, Isa. 60:2. Bwana ataileta njaa ya kuyasikia maneno ya Bwana, Amo. 8:11. Watatokea Makristo wa uongo na manabii wa uongo, Mt. 24:24. Mbwa mwitu wakali wataingia miongoni mwenu, Mdo. 20:29. Nastaajabu kwamba kwa upesi mmeondoshwa kutoka kwake, Gal. 1:6. Kutakuwa na ukengeufu kabla ya Ujio wa Pili, 2 The. 2:3. Baadhi ya watu hukosea juu ya ukweli, 2 Tim. 2:18. Baadhi ya watu wana mfano wa uchamungu lakini wakikana nguvu zake, 2 Tim. 3:2–5. Wakati utafika wakati ambao hawatastahimili mafundisho yenye uzima, 2 Tim. 4:3–4. Patakuwepo na manabii wa uongo na walimu wa uongo miongoni mwa watu, 2 Pet. 2:1. Kuna watu waliojiingiza kwa siri katika kumkana Bwana Mungu pekee, Yuda 1:4. Baadhi ya watu walisema kuwa walikuwa Mitume na hawakuwa, Ufu. 2:2. Nefi aliona kuundwa kwa kanisa lile kuu na lenye machukizo, 1 Ne. 13:26. Wayunani wamejikwaa na kujenga makanisa mengi, 2 Ne. 26:20. Wameenda kinyume na ibada zangu na wamevunja agano langu lisilo na mwisho, M&M 1:15. Giza limeifunika dunia na giza nene limezifunika akili za watu, M&M 112:23. Joseph aliambiwa kwamba makanisa yote hayakawa sahihi; mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu, JS—H 1:19.