Misaada ya Kujifunza
Shadraka


Shadraka

Katika Agano la Kale, Shadraka, Meshaki, na Abednego walikuwa vijana watatu wa Kiisraeli ambao, pamoja na Danieli, waliingizwa katika kasri ya Nebukadneza, mfalme wa Babiloni. Jina la Kiebrania la Shadraka lilikuwa Hanania. Vijana hawa wanne walikataa kujitia najisi wao wenyewe kwa kula nyama na mvinyo wa mfalme (Dan. 1). Shadraka, Meshaki, na Abednego walitupwa na mfalme katika tanuri la moto mkali lakini kimuujiza wakaokolewa (Dan. 3).