Misaada ya Kujifunza
Yohana, Mwana wa Zebedayo


Yohana, Mwana wa Zebedayo

Mmoja wa Mitume Kumi na Wawili katika Agano Jipya, mwana wa Zebedayo, na ni kaka wa Yakobo. Katika maisha yake ya awali yeye alikuwa mvuvi (Mk. 1:17–20). Huenda yeye ni yule mwanafunzi ambaye hakutajwa wa Yohana Mbatizaji aliyetajwa katika Yohana 1:40. Baadaye alipokea wito wa kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo (Mt. 4:21–22; Lk. 5:1–11). Aliandika Injili ya Yohana, nyaraka tatu, na kitabu cha Ufunuo. Alikuwa mmoja wa wale watu watatu walio kuwa na Bwana wakati wa kufufuliwa kwa binti wa Yairo (Mk. 5:35–42), katika Mlima wa Kugeuka Sura (Mt. 17:1–9), na katika Gethsemani (Mt. 26:36–46). Katika maandiko yake yeye mwenyewe anajieleza kama yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu (Yn. 13:23; 21:20) na kama “mwanafunzi mwingine” (Yn. 20:2–8). Yesu pia alimwita yeye na kaka yake kwa jina la Boanerge, maana yake, “wana wa ngurumo” (Mk. 3:17). Kuna marejeo ya mara kwa mara kwake katika taarifa za Kusulubiwa na Ufufuko (Lk. 22:8; Yn. 18:15; 19:26–27; 20:2–8; 21:1–2). Yohana baadaye aliwekwa kizuizini huko Patmo, mahali ambako aliandika kitabu cha Ufunuo. (Ufu. 1:9).

Yohana anatajwa mara kwa mara katika ufunuo wa siku za mwisho (1 Ne. 14:18–27; 3 Ne. 28:6; Eth. 4:16; M&M 7; 27:12; 61:14; 77; 88:141). Mistari hii inathibitisha taarifa iliyoandikwa kibiblia juu ya Yohana na pia inatoa utambuzi wa ukuu wake na umuhimu wa kazi ambayo Bwana amempa kufanya duniani katika nyakati za Agano Jipya na katika siku za mwisho. Maandiko ya siku za mwisho yanafafanua kwamba Yohana hakufa bali aliruhusiwa kubakia duniani kama mtumishi mhudumu hadi wakati wa Ujio wa Pili wa Bwana (Yn. 21:20–23; 3 Ne. 28:6–7; M&M 7).

Nyaraka za Yohana

Ingawa mwandishi wa nyaraka hizi tatu hajitaji mwenyewe kwa jina, lugha inafanana kwa nguvu sana na ile ya Yohana Mtume kwamba inasadikiwa kuwa ameandika zote tatu.

1 Yohana 1 anawaasa Watakatifu kupata ushirika na Mungu. Mlango wa 2 anasisitiza kwamba Watakatifu wamjue Mungu kwa utii na anawafundisha wasiupende ulimwengu. Mlango wa 3 anawaita watu wote kuwa watoto wa Mungu na wapendane. Mlango wa 4 anaelezea kwamba Mungu ni upendo na hukaa ndani ya wale Wampendao. Mlango wa 5 anaelezea kwamba Watakatifu huzaliwa kwa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo.

2 Yohana inafanana na 1 Yohana. Katika hizo Yohana anafurahi kwa sababu ya uaminifu wa watoto wa “bibi mteule.”

3 Yohana anamsifu mtu aliyeitwa Gayo kwa uaminifu wake na kwa msaada wake kwa wale wenye kupenda ukweli.

Injili ya Yohana

Katika kitabu hiki cha Agano Jipya, Yohana Mtume alishuhudia kwamba (1) Yesu ndiye Kristo au Masiya na (2) Yesu ndiye Mwana wa Mungu (Yn. 20:31). Matukio kutoka katika maisha ya Yesu ambayo anayaelezea yamechaguliwa na kupangwa kwa uangalifu kwa kusudi hili. Kitabu kinaanza kwa maelezo ya hali ya Kristo kabla ya kuzaliwa: alikuwa pamoja na Mungu, alikuwa Mungu, na alikuwa ndiye mwumbaji wa vitu vyote. Alizaliwa katika mwili kama Mwana Pekee wa Baba. Yohana anafuatilia historia ya huduma ya Yesu, alisisitiza sana uungu Wake na ufufuko Wake kutoka kwa wafu. Kwa uwazi kabisa anathibitisha kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu, aliyeshuhudiwa kwa miujiza, na mashahidi, na manabii, na kwa sauti ya Kristo mwenyewe. Yohana anafundisha kwa kutofautisha nuru na giza, ukweli na uongo, wema na uovu, Mungu na ibilisi. Pengine hakuna taarifa nyingine iliyoandikwa ambamo ndani yake utakatifu wa Yesu na ukosefu wa imani wa watawala wa Kiyahudi umetamkwa wazi kabisa kama hii.

Yohana aliandika hasa juu ya huduma ya Kristo katika Yuda, hususani wiki ile ya mwisho ya huduma Yake katika mwili wenye kufa, wakati Mathayo, Marko, na Luka waliandika hasa juu ya huduma yake katika Galilaya. Mambo kadhaa kutoka katika injili hii yamefafanuliwa kwa ufunuo wa siku za mwisho (M&M 7 na M&M 88:138–141).

Kwa orodha ya matukio katika maisha ya Mwokozi yaliyoelezwa katika Injili ya Yohana, ona Upatanifu wa Injili katika kiambatisho.

Kitabu cha Ufunuo