Hofu yaweza kuwa na maana mbili: (1) hofu juu ya Mungu ni kujisikia uchaji na heshima Kwake na kutii amri Zake; (2) kumhofia mtu, hatari za kimwili, maumivu, na uovu ni kuwa na woga na mambo ya jinsi hiyo na kuyaogopa sana.
Hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, Mwa. 20:11 .
Nawe utakuwa na hofu na Bwana Mungu wako, Kum. 6:13 (Yos. 24:14 ; 1Â Sam. 12:24 ).
Mtumikieni Bwana kwa hofu, Zab. 2:11 .
Hofu ya Bwana ndiyo mwanzo wa hekima, Zab. 111:10 .
Mhofieni Bwana na mkajiepushe na uovu, Mit. 3:7 .
Itakuwa heri kwao wenye hofu ya Mungu, Mh. 8:12 .
Timizeni wokovu wenu ninyi wenyewe kwa hofu na kutetemeka, Flp. 2:12 .
Mwogopeni Mungu, na mpeni yeye utukufu, Ufu. 14:7 (M&M 88:104 ).
Manabii waliwachochea watu daima ili kuwaweka katika hofu ya Bwana, Eno. 1:23 .
Alma na wana wa Mosia walianguka chini, kwani hofu ya Bwana ilikuja juu yao, Alma 36:7 .
Timizeni wokovu wenu kwa hofu na kutetemeka, Morm. 9:27 .
Wao wasio kuwa na hofu na mimi, nitawasumbua na kuwafanya watetemeke, M&M 10:56 .
Yule mwenye hofu na mimi atazitazamia ishara za kuja kwa Mwana wa Mtu, M&M 45:39 .
Usihofu, kwani mimi niko pamoja nawe, Mwa. 26:24 (Isa. 41:10 ).
Bwana yu pamoja nasi: msiwaogope, Hes. 14:9 .
Usihofu: maana wao walio pamoja nasi ni zaidi, 2Â Fal. 6:16 .
Siwezi kuogopa kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya, Zab. 56:4 .
Msiogope matukano ya watu, Isa. 51:7 (2Â Ne. 8:7 ).
Mungu hajatupa roho wa hofu, 2Â Tim. 1:7 .
Upendo kamili hufukuza hofu, 1Â Yoh. 4:18 (Moro. 8:16 ).
Wana wa Helamani hawakuogopa mauti, Alma 56:46–48 .
Hofu ya mauti huvijaza vifua vya waovu, Morm. 6:7 .
Usiogope mwanadamu anaweza kukutenda nini? Moro. 8:16 .
Usingemwogopa mwanadamu zaidi kuliko Mungu, M&M 3:7 (M&M 30:1, 11 ; 122:9 ).
Usihofu kutenda mema, M&M 6:33 .
Yeyote aliye mali ya kanisa langu hahitaji kuogopa, M&M 10:55 .
Kama mmejiandaa, hamtaogopa, M&M 38:30 .
Jivueni wenyewe katika hofu, M&M 67:10 .
Furahini, na msiogope, kwani Mimi Bwana niko pamoja nanyi, M&M 68:6 .
Msiwaogope maadui zenu, M&M 136:17 .