Misaada ya Kujifunza
Nafsi


Nafsi

Maandiko huzungumza juu ya nafsi katika njia tatu: (1) viumbe roho, kabla ya kuzaliwa katika mwili wenye kufa na baada ya kufa (Alma 40:11–14; Ibr. 3:23); (2) roho na mwili viliungana katika mwili wenye kufa, (M&M 88:15; Ibr. 5:7); na (3) mtu aliye katika mwili usiokufa, mtu aliyefufuka ambaye roho na mwili vimeungana na kamwe haviwezi kutengana (2 Ne. 9:13; M&M 88:15–16).

Thamani ya nafsi

Watu wote ni watoto wa Kiroho wa Mungu. Anamjali kila mtoto Wake na humchukulia kuwa kila mmoja ni muhimu. Kwa sababu ni watoto Wake, wanao uwezekano wa kuwa kama Yeye. Kwa sababu hiyo, ni wa thamani kubwa.