Misaada ya Kujifunza
Simeoni


Simeoni

Katika Agano la Kale, ni mwana wa pili wa Yakobo na mkewe Lea (Mwa. 29:33; 35:23; Ku. 1:2). Aliungana na Lawi katika mauaji ya kinyama ya Washekemu (Mwa. 34:25–31). Unabii wa Yakobo juu ya Simeoni unapatikana katika Mwanzo 49:5–7.

Kabila la Simeoni

Wazao wa Simeoni mara kwa mara waliishi pamoja na kabila la Yuda na ndani ya mipaka ya ufalme wa Yuda (Yos. 19:1–9; 1 Nya. 4:24–33). Kabila la Simeoni liliungana na Yuda katika vita dhidi ya Wakanaani (Amu. 1:3, 17). Pia baadaye waliungana na majeshi ya Daudi (1 Nya. 12:25).