Sheria na matakwa ambayo Mungu huyatoa kwa wanadamu, kwa mtu binafsi au kwa kikundi. Kushika amri za Mungu kutamletea baraka za Bwana na kwa aliye mtiifu (M&M 130:21 ).
Nuhu alifanya kulingana na yale yote ambayo Mungu alimwamuru, Mwa. 6:22 .
Enendeni katika sheria zangu, na kushika amri zangu, Law. 26:3 .
Shika amri zangu, na ukaishi, Mit. 4:4 (Mit. 7:2 ).
Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu, Yn. 14:15 (M&M 42:29 ).
Lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa sababu tunazishika amri zake, 1Â Yoh. 3:22 .
Amri zake si nzito, 1Â Yoh. 5:3 .
Uwe imara katika kushika amri, 1Â Ne. 2:10 .
Bwana hatoi amri isipokuwa amewatayarishia njia, 1Â Ne. 3:7 .
Lazima nifanye kulingana na amri kali za Mungu, Yak. (KM) 2:10 .
Ilimradi mtazishika amri zangu, mtastawi katika nchi, Yar. 1:9 (Alma 9:13 ; 50:20 ).
Jifunze katika ujana wako kuzishika amri za Mungu, Alma 37:35 .
Sielewi, isipokuwa Bwana ameniamuru, Musa 5:6 .
Bwana atawapima wanadamu ili kuona kama watafanya yale yote atakayo waamuru, Ibr. 3:25 .