Misaada ya Kujifunza
Nabii


Nabii

Mtu aliyeitwa na kuzungumza kwa niaba ya Mungu. Kama mjumbe wa Mungu, nabii hupokea amri, unabii, na mafunuo kutoka kwa Mungu. Wajibu wake ni kuyajulisha mapenzi ya Mungu na kuyatambulisha mapenzi na tabia za kweli za Mungu kwa wanadamu na kuonyesha maana ya matendo Yake kwao. Nabii hukemea dhambi na hutabiri matokeo yake. Yeye ni mhubiri wa haki. Wakati mwingine, manabii wanaweza kupata mwongozo kutoka kwa Mungu wa kutabiri mambo yatakayotokea baadaye kwa manufaa ya wanadamu. Wajibu wake wa msingi, hata hivyo, ni kutoa ushuhuda juu ya Kristo. Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ndiye nabii wa Mungu duniani siku hizi. Washiriki wa Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili wanakubalika kama ni manabii, waonaji, na wafunuzi.