Misaada ya Kujifunza
Mambo ya Nyakati


Mambo ya Nyakati

Vitabu viwili katika Agano la Kale. Vinatoa historia fupi ya matukio kutoka Uumbaji hadi tangazo la Koreshi lililowaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu.

Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati

Mlango wa 1–9 inaorodhesha nasaba kutoka Adamu mpaka Sauli. Mlango wa 10 unaelezea kifo cha Sauli. Mlango wa 11–12 inasimulia matukio yanayohusiana na utawala wa Daudi. Mlango wa 23–27 inaelezea kwamba Suleimani alifanywa kuwa mfalme na Walawi wakapangiwa kazi. Mlango wa 28 unaelezea kwamba Daudi alimwamuru Suleimani kujenga hekalu. Mlango wa 29 unandika kuhusu kifo cha Daudi.

Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati

Mlango wa 1–9 ni matukio yanayohusiana na utawala wa Suleimani. Mlango wa 10–12 inaelezea juu ya utawala wa Rehoboamu mwana wa Suleimani, wakati ambao muungano wa ufalme wa Israeli uligawanyika katika falme za kaskazini na kusini. Mlango wa 13–36 inafafanua tawala za falme mbali mbali hadi kukamatwa kwa ufalme wa Yuda na Nebukadneza. Kitabu hiki kinaishia na tangazo la Koreshi kwamba wana wa Israeli walio utumwani wanaweza kurudi Yerusalemu.