Misaada ya Kujifunza
Ghala


Ghala

Mahali ambapo askofu hupokelea, hutunza, na kugawa kwa maskini sadaka zilizowekwa wakfu za Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kila ghala yaweza kuwa kubwa au ndogo kulingana na hali ya mahitaji. Watakatifu waaminifu hutoa vipaji, ujuzi, mali, na fedha kwa askofu ili kuwasaidia maskini wakati wa shida. Kwa hiyo, ghala yaweza kujumuisha orodha ya huduma zinazopatikana, pesa, chakula, au bidhaa nyinginezo. Askofu ndiye wakala wa ghala na hugawa bidhaa na huduma kulingana na mahitaji na kama atakavyoongozwa na Roho wa Bwana (M&M 42:29–36; 82:14–19).