Misaada ya Kujifunza
Malaki


Malaki

Nabii wa Agano la Kale ambaye aliandika na kutoa unabii karibu ya mwaka 430 K.K.

Kitabu cha Malaki

Kitabu au unabii wa Malaki ni kitabu cha mwisho katika Agano la Kale. Kinaelekea kufuatilia mada kuu nne: (1) dhambi za Israeli—Malaki 1:6–2:17; 3:8–9; (2) hukumu zitakazokuja juu ya Israeli kwa sababu ya kutotii kwao—Malaki 1:14; 2:2–3, 12; 3:5; (3) ahadi kwa ajili ya kutii—Malaki 3:10–12, 16–18; 4:2–3; na (4) unabii uhusuo Israeli—Malaki 3:1–5; 4:1, 5–6 (M&M 2; 128:17; JS—H 1:37–39).

Katika unabii wake, Malaki aliandika juu ya Yohana Mbatizaji (Mal. 3:1; Mt. 11:10), sheria ya zaka (Mal. 3:7–12), Ujio wa Pili wa Bwana (Mal. 4:5), na kurejea kwa Eliya (Mal. 4:5–6; M&M 2; 128:17; JS—H 1:37–39). Mwokozi alinukuu milango yote ya Malaki mlango wa 3 na 4 kwa Wanefi (3 Ne. 24–25).