Msaada wa Masomo
Ufunuo
iliyopita inayofuata

Ufunuo

Mawasiliano kutoka kwa Mungu kwenda kwa watoto Wake duniani. Ufunuo waweza kuja kupitia Nuru ya Kristo na Roho Mtakatifu kwa njia ya maongozi ya kimungu, maono, ndoto, au kutembelewa na malaika. Ufunuo hutoa mwongozo ambao unaweza kumwongoza aliye mwaminifu kwenye wokovu wa milele katika ufalme wa selestia.

Bwana huwafunulia manabii Wake kazi Yake na huthibitisha kwa waumini kwamba ufunuo huo kwa manabii ni wa kweli (Amo. 3:7). Kwa njia ya ufunuo, Bwana hutoa mwongozo binafsi kwa kila mtu autafutaye na kwa aliye na imani, mwenye kutubu, na aliye mtiifu kwa injili ya Yesu Kristo. “Roho Mtakatifu ndiye mfunuzi,” alisema Joseph Smith, na “hakuna mtu anayeweza kupokea Roho Mtakatifu pasipo kupokea ufunuo.”

Katika Kanisa la Bwana, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ndiyo manabii, waonaji, na wafunuzi kwa Kanisa na kwa ulimwengu. Rais wa Kanisa ndiye mtu pekee ambaye Bwana amempa mamlaka ya kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa (M&M 28:2–7). Kila mtu anaweza kupokea ufunuo kwa ajili ya manufaa yake yeye mwenyewe.