Misaada ya Kujifunza
Mto Yordani


Mto Yordani

Mto Yordani unatoka katika bahari ya Galilaya hadi Bahari ya Chumvi. Mto huu una urefu wa maili 100 (kilometa 160) na unaundwa kwa muunganiko wa chemchemi kadhaa zinazotiririka kutoka Mlima Hermoni. Ni mto muhimu sana katika Israeli.

Matukio muhimu mawili yanayohusiana na mto huu nayo ni Bwana kuugawanya mto huu kwa ajili ya kuwavusha Waisraeli (Yos. 3:14–17) na ubatizo wa Yesu Kristo (Mt. 3:13–17; 1 Ne. 10:9).