Misaada ya Kujifunza
Zekaria


Zekaria

Nabii wa Agano la Kale aliyetoa unabii mwaka takribani 520 K.K. Aliishi wakati mmoja na nabii Hagai (Ezra 5:1; 6:14).

Kitabu cha Zekaria

Kitabu hiki kinatambulika kwa unabii wake juu ya huduma ya Kristo katika mwili wenye kufa na Ujio Wake wa Pili (Zek. 9:9; 11:12–13; 12:10; 13:6). Mlango wa 1–8 ina mfuatano wa maono ya maisha ya baadaye ya watu wa Mungu. Mlango 9–14 ina maono juu ya Masiya, siku za mwisho, kukusanyika kwa Israeli, vita vikuu vya mwisho, na Ujio wa Pili.