Misaada ya Kujifunza
Uashiriaji


Uashiriaji

Kutumia kitu fulani kama mfano au alama ya kitu kingine. Uashiriaji katika maandiko hutumia vitu vinavyofahamika kiurahisi, tukio, au hali fulani ili kuwakilisha kanuni au fundisho la injili. Kwa mfano, Kitabu cha Mormoni nabii Alma alitumia mbegu kuwakilisha neno la Mungu (Alma 32).

Manabii katika maandiko yote wanatumia uashiriaji kwa kufundisha juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya ishara hizi ni pamoja na sherehe na ibada (Musa 6:63), dhabihu (Ebr. 9:11–15; Musa 5:7–8), sakramenti (TJS, Mk. 14:20–24 [Kiambatisho]; Lk. 22:13–20), na ubatizo (Rum. 6:1–6; M&M 128:12–13). Majina mengi ya kibiblia ni ya kiishara. Sherehe za hema za Agano la Kale na torati ya Musa zilikuwa zinawakilisha kweli za milele (Ebr. 8–10; Mos. 13:29–32; Alma 25:15; Hel. 8:14–15). Kwa mifano mingine ona, Mathayo 5:13–16; Yohana 3:14–15; Yakobo (KM) 4:5; Alma 37:38–45.